Mahakama
moja mjini Cairo imewahukumu kunyongwa wafuasi 529 wa aliyekuwa rais
wa nchi hiyo Mohamed Morsi ambaye aliondolewa na jeshi, ikiwa ni
hukumu inayotolewa baada ya kusikilizwa kwa vikao viwili pekee.
Hukumu
hii ya kifo ni kubwa zaidi kutolewa kwa watu wengi kwa wakati mmoja
kwenye historia ya dunia, hatua ambayo wachambuzi wa mambo wanaona
kuwa mahakama haikufuata mchakato sahihi wa kufikia kutoa hukumu
hiyo.
Huenda
uamuzi huo ukabatilishwa na mahakama ya rufaa kwakuwa mawakili wa
watuhumiwa hao tayari wamewasilisha pingamizi lao dhidi ya hukumu ya
kifo kwa wateja wao wakisisitiza kesi hiy kuchukua muda mfupi zaidi
kuliko kawaida.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire