Pages

jeudi 13 mars 2014

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHINI BURUNDI ATISHIA KUKIFUTA KWENYE ULINGO WA SIASA CHAMA CHA MSD KINACHOONGOZWA NA ALEXIS SINDUHIJE


Waziri wa mambo ya ndani nchini Burundi Edouard Nduwimana

Waziri wa mambo ya ndani nchini Burundi Edouard Nduwimana ametishia kukisimisha au kukifuta kabisa kwenye ulingo wa siasa nchini Burundi chama cha MSD kinachoongozwa na Alexis Sinduhije. Akizungumza kwenye kituo kimoja cha habari nchini Burundi, waziri huyo amesema kifungo numbari 62 cha sheria za vyama vya siasa nchini humo kina mruhusu kufanya hivo, na sasa anasubiri kupata ripoti kutoka tume ya usalama inayo cbhunguza kuhusu yaliojiri siku ya Jumamosi katika makao makuu ya chama hicho ili kuamuwa kuhusu hatma ya chama hicho.

Alexis Sinduhije, mwenyekiti wa chama cha MSD

Wakati huo huo mahakama kuu nchini Burundi imetowa waranti ya kukamatwa kwa mwenyekiti wa MDS Alexis Sinduhije. msemaji wa mahakama Agnes Bangiricenge amesisitiza kuwa Sinduhije anatuhumiwa kuhusu makosa 3, hususan kushiriki katika kundi linalo kaidi taasisi za serikali, Uasi na mashambulizi kwa walinzi wa Usalama wa raia.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...