Alexis Sinduhije, mwenyekiti wa chama cha MSD |
Chama
cha upinzani cha MSD kilicho fungiwa kwa muda wa miezi 4 nchini Burundi
kimemuandikia baruwa katibu mkuu wa serikali ya Burundi kumtaka aunde
tume maalum ya kimataifa ilio huru juu ya kuchunguza vurugu
zilizotokea March 8 mwaka huu kwenye makao makuu ya chama hicho.
Chama
hicho kimesema kipo tayari kushirkiana na tume hiyo ili kuweka wazi
kuhusu ukweli juu ya yaliotokea siku hiyo na kitakubaliana na matokeo
ya tume hiyo.
March
8 mwaka huu kulitokea vurugu kwenye makao makuu ya chama hicho cha
MSD kinachoongozwa na Alexis Sinduhije ambapo watu kadhaa walipoteza
maisha wengine kujeruhiwa huku wengine kutiwa mbaroni.
Kufuatia
vurugu hizo chama hicho kinasema, ukweli lazima utambulike, ili
wahusika wa vurugu hizo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire