Jeshi
la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limedhamiria
kuimarisha usalama katika mji wa Bwegera mtaani Uvira katika jimbo la
kivu kusini baada ya kufanyika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na watu waliojihami kwa silaha, usiku wa kuamkia siku
ya jumatano.
Maafisa
wakijeshi mjini humo wanasema mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya
kupatwa na risasi tumboni mwake huku Mji huo wa Bwegera ukiwa
umegubikwa na Hali ya wasi wasi.
Kamanda
wa Kikosi cha jeshi la serikali ya DRC, FARDC Kanali Elias Rubibi
amelishutumu Kundi la wapiganaji wa kijadi wanaotumia majambia, visu
na mapanga lakini pia ushirikina kwamba ndio wamekuwa wakizorotesha
usalama katika eneo hilo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire