Wakimbizi wa kambi ya Daadab nchini Kenya |
Serikali ya Kenya imeagiza wakimbizi wote walioko nchini humo kurejea kwenye kambi zao za Daadab na Kakuma, agizo linalokuja likilenga kukabiliana na mashambulizi zaidi yanayoshuhudiwa nchini humo.
Waziri
wa ulinzi wa Kenya, Joseph Ole Lenku amewataka wananchi kumripoti
raia yeyote ambaye wanahisi ametoka kwenye kambi hizo na kwamba
atakayebainika kukaidi agizo la Serikali atachukuliwa hatua za
kisheria.
Wakimbizi wa kambi ya Kakuma nchini Kenya |
Tangazo
la Serikali ya Kenya linakuja kufuatia shambulio la siku ya Jumapili
kwenye kanisa moja mjini Mombasa ambao watu wanne walipoteza maisha
kwenye mfululizo wa msahmbulizi ambayo yanadaiwa kufanywa na
wapiganaji wa Somalia ambao baadhi yao wanadaiwa kutoka kwenye
makambi ya wakimbizi toka kwenye taifa hilo.
Nchi
hiyo inakumbwa na mfululizo wa mashambulizi toka ilipotuma wanajeshi
wake nchini Somalia kupambana na wapiganaji wa Al-Shabab.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire