Mkuu
wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton,
amekiri kuwa ziara yake nchini Iran haitoi hakikisho kuhusu kufikiwa
makubaliano ya matumizi ya nyukilia ya taifa hilo.
Kwenye
mkutano wake na wanahabari mjini Tehran punde baada ya kikao chake na
waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif, Ashton
amesema kuwa bado kunasafari ndefu ya kufikiwa suluhu kati ya nchi
hiyo na mataifa ya magharibi.
Ziara
ya Ashton mjini Tehran imekuja ikiwa imepita miezi kadhaa toka
utawala wa Iran chini ya rais mpya, Hassan Rouhani utangaze nia yake
ya kuwa na mazungumzo ya wazi kuhusu mpango wake wa nyuklia na
mataifa ya magharibi na hatimaye kutia saini mkataba wa kuanza
kutekeleza maazimio ya Umoja wa mataifa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire