Mshambuliaji
wa kujitowa muhanga aliyejilipuwa jana jumnne katika mji wa Buula
Burde ulionyakuliwa hivi karibuni kuotka mikononi mwa wanangmabo wa
Alshabab alikuwa ni raia wa Norway mwenye asili ya somalia ambaye
alikuwa na umri wa miaka 60.
Msemaji
wa Al Shabab Abdulaziz Abu Musab ameliambia shirika la habari la
Ufaransa la AFP kwamba mshambuliaji huyo mwenye umro wa miaka 60
anatambulika kwa jina la Abdullahi Ahmed Abdulle ambaye alijiunga na
Al Shabab kutoka Norway kwa ajili ya kupambana na maaduwi wa Allah.
Msemaji
huyo wa Al Shabab amesema mzee huyo amejitolea kwa ajili ya Allah,
ikiwa ni ishara kwamba jihad haina umri.
Hapo
jana, mshambuliaji wa kujitowa muhanga ambaye alikuwa katika gari,
alijilipua kwenye Hoteli ambapo askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika
Amisom kuotka nchini Djibouti walikuwa wamepiga kambi katika mji wa
Buula Burde kwenye umbali wa kilometa 200 na jiji la Mogadishu na
kusababisha mauaji ya askari kadhaa katika tukio hilo.
Mji
wa Buula Burde ilikombolewa kutoka mikononi mwa Al shabab March 13
mwaka huu baada ya majeshi ya Amisom kufanya mashambulizi makubwa na
kuwafurusha wanamgambo wa Al Shabab katika mji huo.
Kundi
la wanamgambo wa alshabab limekuwa likipata pigo kubwa ya kiupoteza
miji muhimu iliokuwa ikikalia tangu mwezi Agosti mwaka 2001 wakati
ilipoanzishwa operesheni ya Amisom dhidi ya wanamgambo hao ambapo
hatuwa ya kwanza ilikuwa ni kufurushwa katika mji wa Mogadishu.
Licha
ya kupoteza miji kadhaa, kundi hilo la Alshab bado linashikilia
maeneo kadhaa ya vijijini na sasa wanapambana kwa kutumia mbinu za
kuendesha mashambulizi ya kujitowa muhanga katika jiji la Mogadishu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire