Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon anataraji kuzuru hivi
karibuni katika nchi nne za ukanda wa Afrika Magharibi zilizo
athiriwa na mlipuko wa Ebola. Ziara hii inakuja wakati nchi ya Sierra
Leone ikiongeza muda wa kampeni ya nyumba kwa nyumba kuhusu Ebola.
Kulingana
na duru za kidiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
atatembelea nchini Liberia, Guinea, Sierra Leone na Mali katika
tarehe mbayo haijatajwa.
Ebola
ambayo ilianza kuzungumziwa kusini mwa Guinea mwezi Desemba mwaka
jana, tayari imegharimu maisha ya watu 6.900 dhidi ya jumla ya watu
watu 18.500 waliodaiwa kuambikizwa virusi ikiwa ni sawa na asilimia
99 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea ikiwa ni takwimu za hivi
karibuni za shirika la Afya duniani WHO.
Nchini
Mali ambako watu saba wameripotiwa kiupoteza maisha kutokana na
Ebola, hali hali bado ni tete licha ya kuondolewa kwa hali ya
uchunguzi dhidi ya watu wanakisiwa kuwa karibu na wahanga wa Ebola
kukutwa hawana virusi hivyo
hayo
yanajiri wakati viongozi wa Sierra Leone wakitangaza kuongeza muda wa
kampeni ya nyumba kwa nyumba juu ya kuhamasisha kuhusu virusi vya
Ebola ambapo kampeni hiyo iliobatizwa "Western Area Surge"
itaendelea hadi Desemba 31.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire