 |
| Askari wa jeshi la Uganda katika kikosi cha Amisom |
Serikali
ya Uganda imeonya kuhusu mbinu mpya zinazopangwa na wapiganaji wa
kundi la Al-Shabab nchini Somalia na kwamba wanamgambo hao wanapanga
kutumia magari ya mafuta kutekeleza uhalifu wao, siku moja baada ya
serikali ya Kenya kubaini bomu kwenye gari moja.
Uganda
inasema imepokea taarofa kuhusu kuwepo mpango wa wapiganaji hao
kutekeleza shambulio mjini Kampala na kwenye nchi zenye wanajeshi
wake nchini Somalia na kwamba wanaongeza usalama.
Tangazo
la Uganda inakuja wakati huu ambapo wapiganaji wa Al-shabab
wameendelea kutekeleza mashambulizi yao dhidi ya wanajeshi wa kulinda
amani na vikosi vya Serikali ya Somalia.
Wakati huo huo taarifa kutoka nchini Somalia zimearifu kuwa watu
kadhaa wamepoteza maisha katika shambulio la kujitowa muhanga
lililotokea katika hoteli moja mjini Buula Burde nchini Somalia, mji
ambao ulirejeshwa mikononi mwa serikali ya Somalia Ijumaa Juma
lililopita baada ya majeshi ya Umoja wa Afrika Amisom kuwafurusha
wanamgambo wa Al Shabab.
Duru
za serikali nchini Somalia zimearifu kuwa askari wanne wa Djibouti
waliomo katika kikosi cha Amisom, wamepoteza maisha katika shambulio
hilo.
Mashahidi
wanasema watu nane wamepoteza maisha baada ya gari lililokuwa
limebeba mabomu kulipuka jana usiku katika hoteli ambayo walikuwa
wamepiga kambi viongozi wa kijeshi wa Amisom kabla ya kufuatiwa na
mashambulizi ya risase.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire