Viongozi
wa kidini nchini jamhuri ya afrika ya kati wameuomba Umoja wa Mataifa
kutuma haraka iwezekanavyo vikosi vya Umoja huo vya kulinda amani
katika nchi hiyo inayoendelea kukumbwa na mzozo wa kivita wenye sura
ya kidini.
Kiongozi
wa kanisa katoliki jijini Bangui Dieudonnee Nzapalanga amesema Jumuiya
ya Kimataifa lazima ifanya jitihada za ziada ili kukomesha machafuko
yanayoendelea kuripotiwa jijini Bangu na vitongoji vyake.
Hivi
karibuni kiongozi huyo wa kanisa katoliki pamoja na Imam wa msikiti
wa Bangui Imam Oumar Kobine Layama na yule wa kanisa la kiprotestanti, wamezuru mataifa
mbalimbali hususan jijini New York Marekani na Italia ambako
walikutana na jamii ya kikatoliki ya San'Egidio ambayo inaunga mkono
juhudi zao.
Hayo
yanajiri wakati mauji yakiendelea kuripotiwa huku na kule jijini
Bangui ambapo hivi majuzi watu zaidi ya sita walipoteza maisha katika
mapigano hayo yenye sura ya kidini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire