Mkuu
wa majeshi wa Misri, Jenerali Abdeli Fattah al-Sisi ametangaza rasmi
kujiuzulu nafasi yake ya ukuu wa majeshi ili kuwania kiti cha urais
kwenye uchaguzi ujao huku akiahidi kupambana na ugaidi iwapo
atateuliwa.
Sisi
ambaye amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuipindua serikali ya
Mohamed Morsi anapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho kwakuwa
hakuna upinzani mkubwa anaotarajiwa kuupata toka kwa wagombea
wengine.
Licha
ya kuungwa mkono na sehemu kubwa ya wananchi wa Misri, hatua yake ya
kuamua kugombea urais kwenye uchaguzi wa mwezi June, kumeleta
mgawanyiko miongoni mwa wananchi ambapo wapo wanaoona kuwa kiongozi
hiyo hakupaswa kuwania kiti hicho na badala yake angebakia kwenye
nafasi yake ya ukuu wa majeshi na waziri wa Ulinzi.
Tayari
baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wanakosoa hatua ya al-Sisi wakisema
uchaguzi hautakuwa huru na haki kwakuwa Serikali yenyewe inayoandaa
uchaguzi huo haikuchaguliwa na wananchi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire