![]() |
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon |
Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ameionya serikali ya Burundi
kuhusu kuendelea kuminywa kwa uhuru wa kujieleza na haki ya kufanya
mikusanyiko ambapo ametoa wito kwa serikali na vyama vya siasa
kujiepusha na haraKati zozote ambazo zinaweza kuchangia kutokea
machafuko.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu Ban, imesema
kuwa kiongozi huyo ameguswa na hali tete ya kisiasa inayoendelea
kushuhudiwa nchini humo kati ya wanaharakati wa upinzani na polisi.
Katibu
mkuu Ban amelaani hatua ya Serikali kukataza mikusanyiko ya kisiasa
ya vyama vya upinzani na hatua ya polisi kutumia nguvu dhidi ya
wapinzani huku kundi la vijana wa chama tawala wakipewa nafasi ya
kufanya mikusanyiko.
Kiongozi
huyo amesema ili nchi ya Burundi ifanye uchaguzi ulio huru na haki
ifikapo mwaka 2015 ni lazima serikali iruhusu uhuru wa demokrasia kwa
kutoa fursa sawa kwa upinzani.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire