Pages

mardi 18 mars 2014

NAVI PILLAY MKUU WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU KWENYE UMOJA WA MATAIFA AZURU NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Navi Pillay mkuu wa tume ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa UN

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay ameanza rasmi ziara ya siku tatu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ambapo atakuwa na mazungumzo na rais Catherine Samba Panza kuhusu machafuko yanayoendelea nchini humo.

Ziara hii ni muhimu kwa Navi Pillay ambaye analenga kuwashawishi viongozi wa taifa hilo kutafuta suluhu ya kitaifa itakayopelekea kumaliza mauaji ya ulipizaji kisasi pamoja na kuwachukulia hatua watu ambao watakuwa wamehusika na mauaji ya kiholela nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Bi Catherine Samba Panza

Ziara hii inakuja wakati huu tayari wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wameanza uchunguzi wao kuhusu mauji ya kidini yanayoendelea kushuhudiwa kwenye taifa hilo kati ya waislamu na wakristo.

Wakati haya yanajiri, wanajeshi wa kulinda amani nchini humo Jumatatu hii wamesema wamefanikiwa kukamata shehena kubwa ya ghala la silaha jirani kabisa na uwanja wa ndege wa mjini Bangui na kwamba wameanza uchunguzi kubaini zilikuwa zinatumiwaje.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...