Suala la Muundo wa Serikali, Madaraka ya rais na Ardhi ni moja kati ya mambo ambayo yanatarajiwa kuwa mjadala mzito wakati wa kikao cha bunge maalumu la katiba mjini Dododma wakati watakapoanza kujadili rasimu ya pili ya katiba baada ya hii leo kuwasilishwa bungeni.
Kufuatia
hapo jana jioni kikao hichi kudumu kwa dakika tatu pekee baada ya
kutokea mvutano wa kuhusu kanuni za bunge maalumu, hatimaye wabunge
hao walikubaliana na hii leo walihudhuria kikao ambacho walipokea
taarifa ya rasimu ya pili ya katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa
tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Sinde Warioba.
Wakati
wa uwasilishaji wake, Jaji Warioba mara kadhaa alilazimika kutumia
muda mwingi zaidi kufafanua masuala nyeti yenye utata ambapo kubwa ni
kuhusu muundo wa muungano na Serikali tatu ambapo zaidi ya asilimia
60 ya wananchi walipendekeza serikali tatu na wachache walitaka
serikali moja.
Suala
jingine ambalo jaji Warioba amesema lilikuwa na mjadala ni lile
linalohusu madaraka ya rais ambapo wananchi walitaka rais apunguziwe
madaraka, na hapa anaeleza mapendekezo ya tume yake.
Haki
ya kumiliki ardhi ni jambo jingine ambalo hata wabunge wenyewe
wanatarajiwa kuwa na mvutano, na hapa jaji Warioba anaeleza ni
kwanini suala la ardhi liingizwe kwenye katiba?
Bunge
maalumu la katiba limeahirishwa hadi siku ya Ijumaa ambapo rais wa
jamhuri ya Muungani wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifungua rasmi
kwa hotuba na sasa wajumbe haop watatumia siku mbili za jumatano na
alhamisi kufanya semina elekezi kuhusu masuala ya katiba kabla ya
kuanza kuijadili rasimu ya pili.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire