Wanajeshi
wa Serikali ya Somalia kwa kushirikiana na vikosi vya kulinda amani
vya Umoja wa Afrika AMISOM, wamefanikiwa kuuchukua mji muhimu wa
Wl-Bur toka kwenye mikono ya wanamgambo wa Al-Shabab.
Mji
huo ulioko umbali wa kilometa 350 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu,
ulikuwa ni ngome muhimu ya wapiganaji wa Al-Shabab waliokuwa
wakiutumia kupanga mashambulizi yao dhid ya vikosi vya Serikali na
vile vya AMISOM.
Kanali
wa jeshi la Somalia, Mohamed Adan amethibitisha vikosi vyao kuingia
kwenye mji huo na kuongeza kuwa wapiganaji hao walikimbia nasasa
wanatekeleza mashambulizi ya kushtukiza toka kwenye maeneo ya misitu
ambako nako wataanza operesheni maalumu ya kuwasambaratisha.
Licha
kwa sehemu kubwa vikosi hivyo kufanikiwa kushikilia miji muhimu toka
kwa wapiganaji wa Al-Shabab, bado wanamgambo hao wameendeleza
mashamblizi makubwa mjini Mogadishu na kutishia hali ya usalama.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire