Bunge
la Somalia hii leo limepokea taarifa rasmi toka kwa balozi wake kwa
nchi ya Kenya, kuhusu operesheni ya kiusalama inayoendelea kufanywa
na vyombo vya Usalama nchini humo na kudaiwa kuwalenga raia wake.
Hapo
jana utawala wa Mogadishu ulimwita nyumbani balozi wake, Mohamed Ali
Nur kwa lengo la kutaka ufafanuzi kuhusu operesheni ya kiusalama
inayoendelea kufanywa na vikosi vya Kenya na kudaiwa kuwanyanyasa
rais wenye asili ya Somalia.
Waziri
wa mambo ya kigeni wa Somalia, Mahad Mohamed Salad amesema hatua hii
ni ya dharura kufuatia taarifa za kukinzana kuhusu operesheni hiyo ya
kenya inayodaiwa kuwalenga raia wa Somalia pekee wanaotuhumiwa
kuhusika na kutekeleza vitendo vya ugaidi nchini humo.
Operesheni
ya vikosi vya usalama vya Kenya imekosolew akwa sehemu kubwa si tu na
wanaharakati wa haki za binadamu bali hata wabunge wa upinzani na
hasa wale wenye asili ya kisomali wanaodai operesheni hiyo inawalenga
raia wa Somalia pekee na wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya
udhalilishaji.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire