Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani makombora yaliyorushwa
kwenye shule moja ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili na kusababisha
mauaji ya raia wa kiPalestina wapatao kumi katika shambulio
lililotekelezwa na askari wa Israeli.
Shambulio
hilo limedhihirisha wazi ukiukwaji mwingine wa sheria za kimataifa
ambapo pande zote mbili zililazimika kulinda usalama wa raia hao wa
Palestina, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na majengo ya Umoja huo,
amesema msemaji wa Katibu Mkuu katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari.
Aidha, msemaji huyo amesisitiza kuwa lazima Makazi ya Umoja wa Mataifa yawe sehemu rasmi ya kukimbilia na si eneo la mapambano kama ilivyojitokeza mara kadhaa na kuwa lazima wahusika wa mashambulio hayo wachunguzwe na kuwajibishwa.
Katibu
Mkuu Ban Ki Moon ameelezea kusononeshwa na ukiukwaji huo wa sheria za
kimataifa na kubainisha kuwa serikali ya Israeli, licha ya kuwa
imefahamishwa maeneo ambapo Umoja wa Mataifa umepiga kambi, askari
wake wanaendelea kutekeleza vitendo vya uhalifu ambavyo Rais wa
Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa havikubaliki.
Tangu
uvunjwaji wa Makubaliano ya kusitisha mashambulizi ya tarehe mosi
Agosti, mamia ya raia wa Palestina tayari wameuwawa kutokana na
mashambulizi hayo huku hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbaya zaidi
katika Ukanda wa Gaza, wakati ambapo Ban Ki-moon akitoa wito wake kwa
pande zote kusitisha mapigano mara moja na kurejelea meza ya
mazungumzo mjini Cairo, Misri.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire