Rais
wa Marekani, Barack Obama, hii leo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa
mkutano wa kimataifa kati yake na viongozi toka barani Afrika,
mkutano uliolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na bara la
Afrika.
Mkutano
huu unafanyika wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo umasikini uliokithiri kwenye baadhi ya
mataifa pamoja na janga la ugonjwa wa virusi vya Ebola ambao
unatishia kusambaa hata kwenye mataifa ya Magharibi.
Rais
Obama anatarajiwa kutumia mkutano huu kuwaeleza viongozi wa Afrika
mkakati wa nchi yake katika kuimarisha biashara na nchi hizo, pamoja
na namna itakavyoendelea kushirikiana na viongozi hao katika vita
dhidi ya kuondoa umasiki na vitendo vya ugaidi.
Takariban
viongozi kutoka nchi 50 ndio wanaohudhuria mkutno huo, ispokuwa pekee
Jamhuri ya Afrika ya kati, Sudani, Eritrea na Zimbabwe ambazo
hazikupewa mualiko, huku Liberia na Guinea zikiahirisha kutokana na
kukabiliwa na gonjwa na Ebola.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire