Mazungumzo
ya amani kuhusu kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan
Kusini yameanza Jumatatu ya wiki hii mjini Addis Ababa, huku
kukishuhudiwa mapigano makali kwenye baadhi ya maeneo.
Wakati
huu wajumbe wa mazungumzo haya wakiendelea kuwasili mjini Addis
Ababa, makundi ya wapiganaji wenye silaha kwenye jimbo la Upper Nile
wamekabiliana na wanajeshi walioasi kwa siku ya pili huku
kukishuhidiwa mfanyakazi mmoja wa shirika la misaada akiuawa kutokana
na mapigano haya.
Tume
ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS imesema kwenye
taarifa yake, kuwa inaguswa na hali ya kuendelea kushuhudiwa kuzorota
kwa usalama nchini humo hasa kwenye miji ya Bunj na jimbo la Upper
Nile ambako kuna zaidi ya wakimbizi laki 1 na elfu 25 wanaotoka
Sudan.
Kwenye
mazungumzo yaliyofunguliwa jana Jumatatu, wapatanishi wa mzozo huo
wamewaonya viongozi wanaohasimiana kuhusu hatua ambazo zitachukuliwa
dhidi yao iwapo mapigano hayatakomeshwa.
Jumuiya
ya maendeleo ya nchi za Afrika mashariki IGAD ambayo ndio
inayosimamia mazungumzo haya imeweka makataa ya hadi kufikia tarehe
10 ya mwezi huu kwa viongozi hawa kufikia makubaliano kuhusu serikali
ya mpito.
Mazungumzo
ya mwisho kati ya rais Salva kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais
Riek Machar yalikwama mwezi June mwaka huu baada ya kila upande
kumtuhumu mwenzake kwa kukiuka mkataba waliotiliana saini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire