Shirika
la kimataifa linalo tetea haki za binadamu lenye makao yake makuu
nchini Marekani la Human Right Watch limelituhumu jeshi la jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo la FARDC pamoja na vikosi vya Umoja wa Mataifa
nchini humo Monusco kwa kupuuzia kuzuia kutokea kwa machafuko ya
mwezi uliopita huko mashariki mwa DRCongo.
Shirika
hilo limesema majeshi ya Congo na yale ya Monusco hayakuingilia kati
ili kukomesha machafuko yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya 30 na
ambayo yalitokea katika kijiji cha Mutarule katika usiku ya Juni 6
kuamkia Juni 7 katika mkoa wa Kivu ya Kusini
shirika
hilo limeendelea kuwa wanajeshi hao waliwaacha wananchi wa Mutarule
waendelee kuuawa wakati ambapo kulikuwa na taarifa za kutokea kwa
machafuko hayo na ambapo wananchi waliomba msaada tangu tu yalipoanza
machafuko hayo na walikuwa karibu wangeliweza kuingilia kati.
Hivi
karibuni kiongozi wa majeshi ya Monusco nchini DRCongo Martin Koble
alibaini maskitiko yake kuona vikosi vya Umoja wa Mataifa vilishindwa
kuziia mauaji hayo yasitokei.
Shirika
hilo limesema hakuna muhusika hata mmoja wa mauaji hayo aliyekamatwa,
hivyo Human rights watch limeilitolea wito jeshi la FARDC na Umoja
wa Mataifa nchini DRCongo Munusco kuchunguza nini kilichotokea na
kuhakikishi mauaji kama hayo hayatokei tena.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire