Pages

vendredi 23 juin 2017

SERIKALI YA BURUNDI YAKIUKA MASHARTI YA UMOJA WA ULAYA

Serikali ya Burundi inaelezwa kukiuka masharti ya kuchukuwa asilimia 20 ya mshahara wa wanajeshi wanaolinda amani nchini Somalia Amisom, kama ilivyokuwa imeafikiana na Umoja wa Ulaya. Mengi zaidi na Ali Bilali

Baada ya mvutano na hatimae kupatikana muafaka, Umoja wa Ulaya ulikubali kutoa malipo ya mshahara wa wanajeshi wa Burundi walipo katika kikosi cha Umoja wa Afrika wanaolinda amani nchini Somalia Amisom, baada ya kukubaliana masharti mawili na serikali ya Burundi.

Sharti la kwanza ilikuwa ni pesa hizo kutopitia kwenye Benki kuu ya taifa, badala yake ziwekwe kwenye akaunti ya benki binafsi, wakati sharti lingine ni serikali ya burundi kutokata asilimia 20 ya mshahara huo wa wanajeshi kama ilivyokuwa imezoeleka.

Umoja wa Ulaya umeanza kutoa pesa hizo tangu kipindi kadhaa, ambazo zinapitia kwenye benki binafasi kama ilivyoasfikiwa katika makubaliano na serikali ya Burundi, lakini wanajeshi wanaofaidi na hatuwa hiyo hata hivyo wamesema hakuna kilichobadilika.

Hata hivyo wazara ya ulinzi nchini Burundi ilikuwa imefahamisha awali kwamba wanajeshi wote walipo nchini Somalia, watapokea mishahara yao kupitia akaunti za ushirikiano wa kijeshi ama cooperative militaire ambazo jeshi linadhibiti kwa asilimia mia moja.

Duru za kidiplomasia zinaeleza kwamba Umoja wa Ulaya umekeisha lipa malimbikizo ya mwaka mzima ya wanajeshi hao ambao wao wanasema wamekewisha pokea malimbikizo ya mshahara wa miezi mitano pekee na bado wanakatwa asilimia 20

msemaji wa jeshi la Burundi Gaspard baratuza amesema wanajeshi wenyewe ndio waliokubali kuchangia wenyewe ili kusaidia kuendelea kwa harakati za kulinda amani nchini Somalia, jambo ambalo limepingwa vikali na wanajeshi

Umoja wa Ulaya haijazungumza lolote kuhusu swala hili nyeti na lenye utata.





Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...