JIM MATTIS waziri wa Ulinzi wa Marekani |
Waziri
wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu hapo jana amefanya
mazungumzo na mfalme wa Qatar, mazungumzo ambayo yalilenga kuendelea
kujaribu kutafuta suluhu kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya
Ghuba wakati huu pia umoja wa Mataifa ukieleza kuguswa na hali
inayoendelea.
Haya
yanajiri wakati huu nchi ya Marekani kupitia kwa waziri wake wa mambo
ya Kigeni Rex Tillerson akizikosoa nchi za Ghuba kwa kukitangaza
chama cha Muslim Brotherhood kama kundi la kigaidi wakati kipo karibu
kwenye nchi zote za Ghuba na baadhi ya wafuasi wake ni viongozi.
Miongoni
mwa vikwazo vilivyotangazwa dhidi ya Qatar ni pamoja na nchi hiyo
kutakiwa kuacha ufadhili wake kwenye chama cha Muslim Brotherhood.
Katika
hatua nyingine waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis na mwenzake wa
Qatar Khalid al-Attiyah wametiliana saini makubaliano ya nchi hiyo
kuiuzia Qatar ndege za kivita zenye thamani ya dola bilioni 12.s
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire