Mtu
mmoja ameuawa jana jioni jijini Bujumbura katika kata ya Musaga,
baada wahalifu kuvurumisha guruneti iliowajeruhi pia watu kadhaa.
Kwa
mujibu wa msemaji wa polisi nchini humo Pierre
Nkurikiye, guruneti hiyo ilrushwa karibu na kituo cha mafuta majira
ya saa kumi na mbili saa za Bujumbura na kusababisha kifo cha dereva
mmoja wa gari huku watu wengine tisa wakijeruhiwa.
Inahofiwa
idadi ya waliopoteza maisha kuongezeka kufuatia baadhiya majeruhi
ambao walijeruhiwa vibaya.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire