Wachunguzi
wa Umoja
wa Mataifa wanasema kuwa vyombo vya usalama nchini Burundi na
wapiganaji wanaoshirikiana na Serikali wameendelea kutekeleza vitendo
vya mateso na kuua wapinzani, tuhuma ambazo zinakanushwa vikali na
Serikali.
Wachunguzi
hao kutoka tume ya umoja wa Mataifa iliyopewa jukumu la kuchunguza
matukio ya ukiukwaji wa haki za Binadamu nchini Burundi walinyimwa
kibali cha kuingia nchini humo ambapo wamesema kuna vitendo vingi vya
ukiukaji wa haki za binadamo vinavyofanywa na Serikali na washirika
wake.
Tume
hiyo imesema kuwa baada ya kuwahoji zaidi ya raia 400 waliokimbia
nchi yao, wamethibitisha pasipo na shaka hofu waliyokuwa nayo toka
awali kuhusu vitendo vya unyanyasaji vinavyotekelezwa na Serikali ya
Burundi.
Serikali
ya Burundi kwa upande wake tayari imesema haikubaliana na matokeo ya
uchunguzi wa kamati hii na kwamba imelenga kwa makusudi kutaka
kuwapeleka maofisa kadhaa wa Serikali kwenye mahakama ya uhalifu wa
kivita ya ICC.
Tume
hii iliundwa mwaka 2016 ilipewa jukumu la kuchunguza na kuamua ikiwa
kuna watu wanapaswa kuwajibishwa kutokana na tuhuma za ukiukaji wa
haki za binadamu na uhalifu dhidi ya binadamu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire