Mwendesha
mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC
ametoa wito wa kukamatwa na kujisalimisha kwa mtoto wa kiongozi wa
zamani wa Libya marehemu kanali Muammar Gaddafi, Seif al-Islam
aliyeachiwa juma lililopita kutoka kwenye gereza la Zintan alikokuwa
anashikiliwa.
Mwendesha
mashtaka Fatou Bensouda amesema kuwa hati ya kukamatwa kwa Seif
al-Islam iliyotolewa na mahakama hiyo mwaka 2011 bado ni halali na
viongozi wa Libya wanawajibika kumkamata licha ya msamaha wowote
aliopewa nchini humo.
Seif
al-Islam aliripotiwa kuachiwa huru Ijumaa ya wiki iliyopita na waasi
wa eneo la Zintan, kundi ambalo lilikuwa likimshikilia kwa zaidi ya
miaka mitano ambapo lilitangaza kumuachia huru kwa msamaha katika
kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadan.
Hata
hivyo ofisi ya mwendsha mashataka wa ICC iliyoko mjini Tripoli Libya
ambako iko Serikali inayotambuliwa kimataifa, imesema kuwa msamaha
huo hauwezi kumuhusu Seif al-Islam kwa sababu tu ya aina ya makosa
anayotuhumiwa nayo.
Bensouda
amesema Seif al-Islam anatakiwa na mahakama hiyo kwa tuhuma za makosa
ya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na kwamba hivi sasa
wanajaribu kujua mahali aliko.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire