Rais
wa Rwanda Paul Kagame, amebaini maskitiko yake kufuatia tukio la hivi
karibuni katika eneo la Rusizi sekta ya Bugarama, ambako watu wenye
silaha walishambulia na kusababisha mauaji ya mtu mmoja na kuwajeruhi
wengine nane.
Taarifa
zinaeleza kwamba washambuliaji waliingia katika baa moja katika
kijiji cha Ryankana na kuanza kupigia risase wakifuatisha na
guruneti, tukio ambalo msemaji wa polisi nchini Rwanda Rene
Nkendabanga juma hili alieleza kwamba linafanana na tukio liliotkea
miezi kadhaa iliopita ambapo watu kutoka Burundi waliashambulia na
kusababisha mauaji kabla ya kutokomea.
Rais
Kagame amesema matukio hayo hayawezi kuendelea, lazima yapatiwe
suluhu la haraka.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire