Kamati
ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema kuwa wafanyakazi wake wawili
waliotekwa nyara na kundi la watu wenye silaha mashariki mwa nchi ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo juma lililopita, wameachiwa huru.
Wafanyakazi
hao walitekwa nyara Juni 7 katika eneo la kati ya mji wa Kirumba na
Beni kaskazini mwa jimbo la Kivu Kaskazini wakati walipokuwa kwenye
operesheni za kibinadamu, hatua iliyoilazimu kamati hiyo kusitisha
huduma zake kwenye eneo hilo ikitaka kwanza wafanyakazi wake
waachiwe.
Msemaji
wa kamati hiyo Christine Cipolla amethibitisha kuachiwa kwa
wafanyakazi wao na kuongeza kuwa wamepata ahueni lakini
wanasikitishwa na kuendelea kuongezeka kwa vitendo vya utekaji nyara
kwenye eneo la mashariki.
Kamati
hiyo imesema kuwa makataa yake ya kuhudumia eneo la mashariki bado
itaendelea ambapo ilikuwa ikihudumia zaidi ya familia elfu 5.
Eneo
la Kivu Kaskazini kwa muda mrefu limekuwa kitovu na makazi ya
wapiganaji wa Kihutu wa FDLR wa nchini Rwanda toka mwaka 1994 na
limekuwa likiendesha vitendo vya utekaji nyara na kutatiza usalama
mashariki mwa nchi hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire