Wananchi
wa Uingereza wameendelea kuonesha hasira zaid dhidi ya Serikali
wakitaka majibu ya kina kuhusu chanzo kilichosababisha moto mkubwa
kwenye jengo moja mwanzoni mwa juma hili ambapo watu 17 walipoteza
maisha huku miili mingine ikishindikana kutambuliwa kutokana na
kuungua vibaya.
Meya
wa jiji la London Sadiq Khan alijikuta matatani baada ya kundi la
wananchi kumvamia na kuhoji hatua gani zitachukuliwa dhidi ya
wamiliki wa jengo hilo na wengine wakitaka majibu ya chanzo cha moto
huo.
Waziri
mkuu Theresa May tayari ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina
kuhusu chanzo cha moto huo pamoja na wamiliki wake kuhojiwa akiahidi
hakuna atakayeachwa kwenye uchunguzi huo.
Juma
hili jengo la Ghorofa 24 kwenye eneo la Grenfell liliwaka moto na
kuziacha mamia ya familia zikiwa hazina mahali pa kuishi na wengine
kupoteza ndugu zao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire