Watu
sita wameripotiwa kufa na wengine mamia wamejeruhiwa baada ya mtu
aliyejitoa muhanga kwa kutumia gari kulenga mgahawa mmoja maarufu
ulioko mjini Mogadishu, Somalia wakati watu wakiwa wanakula futari.
Polisi
mjini Mogadishu imethibitisha kutoke kwa tukio hilo ambalo imesema
kuwa mtu aliyejitoa muhanga aliendesha gari lililokuwa na vilipuzi
ndani ya jengo ambalo mgahawa wa Posh Treat ulikuwa umesheheni
waumini wa dini ya kiislamu.
Afisa
wa polisi Abukar Mohamed amethibitisha kuuawa kwa watu sita na
wengine kadhaa kujeruhiwa na kuongeza kuwa operesheni ya kukagua
jengo hilo imeendelea usiku kucha huku eneo lote la mgahawa huo
likiwa limefungwa.
Kundi
la Al-Shabab ambalo lina uhusiano na mtandao wa kigaidi wa AL-Qaeda
kundi ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara
mjini Mogadishu kuvilenga vikosi vya Serikali na vile vya kigeni,
limekiri kuhusika kwenye shambulio hili.
Mara
nyingi wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadan kundi la Al-Shaba
limekuwa likizidisha mashambulizi yake nchini Somalia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire