Wakati
mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi yakionekana kukwama, risala
inayoonekana kuwa ya siri ya mratibu wa mazungumzo kwa viongozi wa
nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki katika mkutano wa Mei 20,
inatembea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ali Bilali
anatudokzea yaliomo kwenye hotuba hiyo.
Katika
risala hiyo iliovuja, Benjamin Willima Mkapa ambae sio mara nyingi
kuzungumzia shughuli zake katika mazungumzo ya Warundi, ametaja
matatizo kadhaa anayo kabiliana nayo katika juhudi za kuwaleta pamoja
wanasiasa wa Burundi.
Tangu
kukabidhiwa jukumu zito la kuwaleta pamoja wanasiasa wa Burundi,
mratibu wa mazungumzo Benjamin Mkapa, ameandaa vikao mara tatu mjini
Arusha, vikao ambavyo havikuzaa matunda yoyote hadi sasa.
Mwaka
mmoja tangu uteuzi huo msuluhishi katika mzozo huo hajafaulu kuzileta
pamoja pande zote katika mgogoro wa Burundi, amekuwa akikutana nao
kwa nayakati tofauti na ambapo wamekuwa wakimpa maoni ambayo
inaonekana imekuwa vigumu kuyaweka pamoja.
Seriali
ya Burundi inashikilia msimamo wake kwamba nchi ni tulivu, mazungumzo
lazima yafanyike nchini Burundi na imeanza mchakato wa manadiliko ya
katiba, jambo ambalo linatupiliwa mbali na upinzani unaodai kuwa
usalama ni mdogo huku watu wakitiwa nguvuni kiholela, matukio ya
utesaji, unyanyasaji, na watu wanaotoweka katika mazingira tatanishi.
Neno
msuguano limerejea mara nyingi katika risala hiyo ambapo serikali
imeelezwa kuwajibika katika kusuasua kwa mazungumzo hayo. Mratibu
anawataka viongozi wa serikali kuonyesha dhamira ya dhati kwa kufuta
waranti ya kukamatwa kwa viongozi wa upinzani na wa mahirika ya
kiraia, kuwaacha huru wafungwa na kukubali kuzungumza na makundi
yanayo shikilia silaha.
Katika
kutamatisha risala hiyo ya siri, Benjamin Mkapa ameeleza ofisi yake
imeathirika mara kadhaa na uvujishwaji wa taarifa. Na kukumbusha
kwamba baadhi ya nyaraka huwasilishwa kwa sekretarieti ya jumuiya ya
Afrika mashariki.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire