Serikali
ya Tanzania kupitia waziri wake wa habari Dr Harrison Mwakyembe
imetangaza kulifungia gazeti la MAWIO kwa muda wa miaka miwili baada
ya gazeti hilo kuchapisha habari iliyowahusisha marais wastaafu na
ripoti ya madini iliyokabidhiwa kwa rais Magufuli Jumatatu ya wiki
hii.
Juma
hili rais Magufuli alivionya vyombo vya habari kuhusu kuwahusisha
viongozi hao na taarifa za uchunguzi wa sakata la madini
alizokabidhiwa ikulu.
Serikali
inasema viongozi hao hawakutajwa popote kwenye ripoti ya uchunguzi na
hivyo kuwahusisha na ripoti hizo ni kutaka kuwachafua viongozi hao.
Akitoa
tangazo hilo mkurugenzi wa idara wa Idara ya Habari Maelezo, Dr
Hassan Abbasi amesema hatua zilizochukuliwa zimezingatia sheria mpya
ya huduma za habari.
Gazeti
la MAWIO liliandika habari iliyoambatana na picha za marais wastaafu
Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete habari yenyewe ikiwahusisha viongozi
hao na ripoti ya uchunguzi wa madini iliyowasilishwa kwa rais
Magufuli.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire