Rais
wa Marekani amewajibu kwa hasira wakosoaji wake baada ya kuchapishwa
kwa ripoti kwenye gazeti la Washington Post ikieleza kuwa
anachunguzwa na tume maalumu kuhusu kutaka kupindisha sheria katika
kile alichokiita “utafutaji wa mchawi” unaoongozwa na watu wabaya
dhidi yake.
Trump
alikuwa akijibu tuhuma dhidi yake ambapo anadaiwa kuwa tayari
uchunguzi rasmi umeanzishwa dhidi yake huku mwenyewe akikosoa namna
ambavyo wakosoaji wake wamedhamiria kumlenga kwa tuhuma ambazo hazina
msingi.
Licha
ya kuwa rais Trump hakuzungumzia moja kwa moja tuhuma zinazomkabili,
lakini akaeleza kuwa kinachoendelea hakijawahi kushuhudiwa kwenye
historia ya Marekani kwa rais kushambuliwa kwa wakati mmoja.
Rais
Trump amesema walitengeneza habari kuhusu kushirikiana na Urusi
kwenye uchaguzi uliopita lakini hawakupata ushahidi na sasa wameamua
kuchunguza kuhusu uwezekano wa kutaka kupindisha sheria.
Hata
hivyo kamati inayochunguza sakata hili haijaweka wazi ikiwa kweli
inamchunguza rais Trump.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire