Waziri wa habari nchini Nigeria Lai Mohamed |
Siku nne baada ya kutokea kwa shambulio katika shule moja mjini Dapchi nchini Nigeria, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika mji huo uliopo kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako vikosi vya usalama vimekabiliana na wananchi wenye hasira ambao hadi sasa hawajuwi wapi walipo binti zao.
Polisi imethibitisha kuwa wasichana 111 wa shule la wasichana mjini Dapchi wametoweka tangu kutokea kwa shambulio la kundi la kijihadi la Boko Haram
hofu imeendelea kutanda katika eneo hilo ikihofiwa kutokea kwa Chibok mpya, jimbo lililopo jirani na mji wa Borno ambako kundi la Boko Haram liliwateka wasichana 276 April mwaka 2014, tukio lililolaaniwa ulimwengu mzima.
Ujumbe wa serikali ukiongozwa na waziri wa habari Lai Mohamed ulielekea katika eneo hilo na hivyo kuzua hasira miongoni mwa wananchi ambao wanasema hawajuwi nani wa kuwapa msaada.
Hivi majuzi watu wenye silaha walivamia mji huo na kusababisha mtafaruku mkubwa.
Waziri wa ulinzi nchini Nigeria Jenerali Mansour Dan Ali amesema wasichana wengi walikimbia kutokana na uoga na baadhi wameanza kurejea shuleni.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire