Mamlaka
nchini Uturuki zimeendelea na operesheni ya kuwasaka na kuwakamata
watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi lililoshindikana, dhidi ya Rais
Racep Tayyip Erdogan, ambapo mpaka sasa watu zaidi ya elfu 6
wanashikiliwa, huku Serikali ikiapa kumaliza kile ilichokiita
“Virusi”.
Hapo
jana wakati rais Erdogan akihudhuria ibada maalumu ya mazishi
kuwakumbuka raia na wanajeshi waliouawa wakati wa jaribio la
mapinduzi, amesema kuwa nchi yake inafikiria upya kurejesha adhabu ya
kifo, licha ya wasiwasi ulioneshwa na jumuiya ya Kimataifa.
Viongozi
wa dunia, akiwemo Rais wa Marekani, Barack Obama, wamealaani jaribio
la mapinduzi lililoshindikana Ijumaa ya wiki iliyopita na wanajeshi
walioasi, ambapo kwa mujibu wa Serikali watu zaidi ya 300 waliuawa.
Hata
hivyo kumekuwa na hofu ya kutekelezwa vitendo vya ukiukwaji wa haki
za binadamu kwa watuhumiwa wa jaribio hilo, baada ya kuonekana kwa
picha zikiwaonesha maofisa wa Serikali wakiwanyanyasa wanaodaiwa kuwa
ni watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi.
Waziri
wa sheria wa Uturuki, Bekir Bozdag, amesema kuwa watu wanaokadiriwa
kufikia elfu 6 wamekamatwa katika operesheni maalumu ya kusafisha
jeshi na taasisi za Serekali ambazo anadai zimevamiwa na watu
wanaotaka kutekeleza mapinduzi, huku akionya kuwa idadi hiyo huenda
ikaongezeka.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire