Viongozi wa Umoja wa Afrika wanajdili kuhusu usalama wa Sudani Kusini na Burundi ambako mzozo wa kisiasa umeendelea kutokota katika nchi hizo, na ambapo mwenyekiti wa Umoja huo amewatolea wito viongozi wa mataifa hayo kuheshemu makubaliano na mikataba mbalimbali iliofikiwa.
wakati huo huo rais
wa Sudan Kusini, Salva Kiir na makamu wake wa kwanza wa Rais Riek
Machar, wamekubali kukutana kwa mazungumzo, ili kusaka muafaka wa
kurejesha amani nchini humo, baada ya mapigano yaliyoshuhudiwa juma
moja lililopita.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa tume inayosimamia utekelezwaji wa mkataba wa
amani uliotiwa saini na viongozi hao kumaliza vita nchini humo,
Festus Mogae, amethibitisha Rais Kiir kuzungumza kwa njia ya simu na
Riek Machar na kukubaliana kukutana, wakati huu pia jumuiya ya nchi
za IGAD, ikifikiria kutuma wanajeshi elfu 14 nchini Sudan Kusini
kulinda amani.
Viongozi Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika,
wanaotarajiwa kutamatisha kikao chao hivi leo jijini Kigali, Rwanda, wanatarajiwa kutoka na maazimio kuhusu kinachoshuhudiwa kwenye
nchi hiyo.
Hata
hivyo maswali bado ni mengi ikiwa kweli wakuu hawa wa nchi wana nia
ya dhati ya kumaliza machafuko Sudan Kusini, na kama watatoka na
maazimio mahsusi kumaliza mgogoro wa nchi hiyo.
Haji
Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa, akiwa jijini Dar es
Salaam, Tanzania na hapa anaeleza mtazamo wake.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire