Pages

lundi 14 décembre 2015

MAREKANI YAWATAKA RAIA WAKE KUONDOKA BURUNDI

Serikali ya Marekani imewataka raia wake wanaoeshi nchini Burundi kuondoka mara moja nchini humo kufuatia kuendelea kuhatarishwa kwa hali ya usalama nchini humo tangu pale lilipofeli jaribio la mapinduzi mwezi Mei mwaka huu lililofuatiwa na machafuko na mzozo wa kisiasa.

Katika taarifa ya wizara ya mambo ya nje wa Marekani hapo jana imewataka raia wa Marekani wasiokuwa na shughuli muhimu kuondoka nchini humo na familia zao na kuwataka raia wote wa Marekani kutoelekea Burundi, na wale waliopo nchini humo kuondoka haraka iwezekanavyo.

Zaidi ya watu 90 wameuawa siku ya Ijumaa Juma lililopita baada ya kutokea kwa mashambulizi ya kambi tatu za kijeshi nchini humo, ambapo taarifa za jeshi la nchi hiyo ziliarugu kuuawa kwa waasi 79 na wanajeshi 8.

Jumamosi asubuhi maiti kadhaa zilizshuhudiwa katika mitaa ilioendesha maandamao ya kupinga muhula wa 3, ambapo wengi wa waliouwawa ni vijana. Mashuhuda nchini humo wamevituhumu vikosi vya Usalama kuwashikilia vijana waliokutana nao baada ya shambulio la kambi za kijeshi na kuwauwa, ambapo maiti kadhaa zilionekana zikifungwa kamba mikononi.

Kulingana na taarifa ya pamoja ua mjumbe wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini na kamishna wa ushirikiano wa kimataifa Neven Mimica wameomba ukweli uwekwe wazi kuhusu mauaji haya yanayotokea katika karne hii.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...