Kundi la wanamgambo wa Al Shabab, limejigamba kuhusika katika shambulio la bomu lililo gharimu maisha ya Watu
sita na wengine kadhaa wamejeruhiwa
katika shambulio hilo la bomu lililotegwa kwenye gari mjini Mogadishu
nchini Somalia,.
Polisi
mjini Mogadishu wamethibitisha kutokea kwa shambulio hilo na kuongeza
kuwa lilitekelezwa kwenye lango kuu la kuingia kwenye uwanja wa ndege
wa mjini Mogadishu ambako pia kuna ngome ya vikosi vya majeshi ya
kulinda amani ya Umoja wa Afrika AMISOM.
Kwa
mujibu wa taarifa za awali za polisi zinasema kuwa, mtu aliyetekeleza
shambulio hilo alipaki gari jirani na kituo ukaguzi cha kuingia
kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu na wakati akikaribiwa kukaguliwa
alijilipua na kusababisha vifo vya watu 6.
Mbali
na eneo hilo kuwa ngome ya vikosi vya AMISOM pia ni jirani kabisa na
ofisi za ubalozi wa Uingereza nchini Somalia pamoja na ofisi kadhaa
za mashirika ya kimataifa ambayo yako nchini humo kukabiliana na
wapiganaji wa kundi la Al-Shabab.
Mpaka
sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika kwenye shambulio
hilo, ingawa kuna kila dalili kuwa huenda wapiganaji wa Al-Shabab
wenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda wakawa wamehusika na shambulio
hilo kufuatia mashambulio yao ya hivi karibuni mjini Mogadishu
wakilenga vikosi vya kulinda amani na raia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire