Pages

lundi 10 février 2014

MAREKANI YAZIONYA PANDE ZINAZOHUSIKA NA MZOZO NCHINI SUDANI KWA KUKIUKA MKATABA WA KUSITISHA VITA



 Marekani imeonya na kutahadharisha juu ya mustakabali wa Sudani Kusini na kusema kuwa serikali na upande wa waasi wanaendelea kuiweka nchi hiyo katika hali ya migogoro na vita kutokana na kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya watu wengi.









Kauli hiyo ya Marekani inakuja wakati waangalizi wa hatua ya kusitishwa kwa mapigano kutoka Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki, IGAD wakiwa nchini humo kutathimini utekelezwaji wa makubaliano hayo yaliyofikiwa mwezi uliopita kati ya waasi na serikali.

Marekani imesema kuwa inaguswa na hali ya machafuko nchini Sudan Kusini na kuzishushia lawama pande hizo mbili kutokana na kukiuka makubaliano ya Addis Ababa.

Hayo yanajiri wakati serikali ya Sudan Kusini ikisema kuwa ipo tayari kwa mazungumzo ambayo yanatarajiwa kuanza huko Addis-Ababa Ethopia na kundi la waasi kwenye juhudi za kusaka suluhu la amani ya kudumu nchini humo pia imesema kuwa kwa sasa inadhibiti majimbo yote, baada ya kuyaweka kwenye himaya yake majimbo yaliyokuwa chini ya udhibiti wa waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamo wa rais wa taifa hilo changa, Riek Machar.


Hata hivyo upande wa waasi umekanusha madai hayo 

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...