Hali
ya taharuki imeendelea kutanda jijini Kinshasa karibu na biunge la
taifa nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako polisi ya
usalama imeendelea kuewatawanya wafuasi wa upinzani wanaopinga mpango
wa mageuzi ya sheria ya uchaguzi ambayo ilipangwa kujadiliwa bungeni
hii leo.
upinzani
nchini drcongo unaona kwamba mageuzi ya sheria hiyo ya uchaguzi
yatachelewesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa rais utaompa nafasi
rais wa sasa wa nchi hiyo Joseph Kabila madarakani tangu mwaka 2001
kuendelea kusalia uongozini baada ya kutamatika kwa muhula wake wa
tatu na wa mwisho mwaka 2016.
polisi
wa usalama wa raia wamezuia maeneo yote yanayoelekea kwenye majengo
ya bunge la taifa nchini humo Palais du peuple ambako wabunge
walipanga kujadili muswada wa sheria uhusuo mabadiliko ya sheria ya
uchaguzi uliowasilishwa bungeni na serikali kwa ajili ya kujadiliwa
katika kikao cha bunge mchana huu.
Katika
taarifa ya awali wabunge wa upinzani waliafifu kwamba watasusia cikoa
hivyo vya kufanya mageuzi katiba ya nchi hiyo katika kile
walichokiita kuhofia kuwa wahaini.
Mapema
leo asubuhi polisi wamewasambaratisha wafuasi wa upinzani takriban
300 hivi waliokuwa wamekusanyika karibu na ofisi za bunge kwa kutumia
bomu za kutowa machozi, kabla ya kukimbilia kwenye ofisi za vyama vya
upinzani hususan chama cha UNC cha Vital Kamerhe ambako kumeshuhudiwa
mvutano wa polisi na vijana waliochoma moto magurudumu.
Israel
Mutombo Msemaji wa kiongozi wa polisi nchini humo jenerali Celsstin
Kanyama amesema wamekuhamasisha idadi kubwa ya polisi nchini na
kwamba hawana habari yoyote kutoka serikali inayoruhusu kufanyika kwa
maandamano.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire