Mashambulizi
ya kigaidi yaliotokea jijini paris nchini Ufaransa juma lililopita
yamezua hisia tofauti kwa viongozi wa ulaya juu ya swala la
kushirikiana katika kuzidisha ulinzi wa kuzuia kutokea kwa
mashambulizi zaidi ya kigaidi katika bara la Ulaya.
Hata
hivyo kumekuwa na hali ya kutoelwana kuhusu swala hili la kubadilisha
taarifa katika ya mataifa ya bara la ulaya ambapo bunge la umoja wa
ulaya linahofia kuwanyima haki ya kutembea wananchi kutoka katika
maeneo hayo.
Miongoni
mwa hatuwa hizo ni kurekebisha sheria za kusafiri katika eneo la
Shengen, kufanya upekuzi zaidi kwa baadhi ya abiria, kuorodhesha
katikas kitabu maalum wasafiri, kupeana taarifa za kijasusi kati ya
mataifa ya Ulaya, kudhibiti matumizi ya mitandao ya Internet na
kuzuia kuzagaa kwa silaha.
Hii
si mara ya kwanza viongozi wa ulaya wanazungumzia kuhusu swala hili,
lakini mara zote wameshindwa kukubaliana.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire