Polisi
nchini Tanzania imeanza uchunguzi kuhusu tukio la kujipiga risasi na
kufa kwa kaimu balozi wa Libya nchini humo, Ismail Nwairat.
Kamishna
wa kanda maalumu ya dar es Salaam, Suleimani Kova amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari kikosi cha askari wa
upelelezi wameanza uchunguzi kuhusiana na tukio hili.
Kwa
mujibu wa wizara ya mambo ya nje nchini humo na mkurugenzi wa idara
ya habari maelezo Assa Mwambene, amesema balozi Nwairat alijipiga
risasi mwenyewe akiwa kwenye chumba cha ofisi yake ambapo wafanyakazi
wa ubalozi walilazimika kuvunja mlango ili kujua kilichotokea.
Ubalozi
wa Libya nchini Tanzania umethibitisha kifo cha kaimu balozi wake na
kuongeza kuwa mipango imeanza ya kuusafirisha mwili wake kwenda mjini
Tripoli.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire