Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamuwa kuliwekea vikwazo kundi la
waasi wa Uganda la ADF lililopiga kambi mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo. Vikwazo hivyo vitawahusu viongozi wa kundi
hilo kuwazuia kusafiri na kuhodhi fedha zao.
Vikwazo
hivyo vilipendekezwa na mataifa ya Ufaransa, Marekani na Uingereza.
ADF linaongozwa tangu mwaka 2007 na Jamil Mukulu ambaye alikuwa
mkristo kabla ya kuslim kuwa muislam pamoja na kiongozi wa kijeshi
Hood Lukwago ambao wamewekwa katika orodha ya viongozi wa makundi ya
kigaidi na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya.
Kundi
la ADF ambalo pia linatambulika kwa jina la ADF-NALU linatuhumiwa
kuwasajili watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 katika kundi hilo
na kutekeleza mauaji lakini pia ubakaji dhidi ya kinamama na watoto
na kuwashambulia wanajeshi wa kulinda amani nchini DRCongo Monusco.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire