Pages

lundi 30 juin 2014

BOKO HARAM LASHUKIWA KUTEKELEZA MAUAJI NA KULENGA MAKANISA


Watu kadhaa waumini wa kikrisoto wamepoteza maisha wakiwa kanisani na wengine wakati wakijaribu kutoroka hapo jana Jumapili katika shambulio linalo shukiwa kuwa limeendeshwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Makanisa kadhaa yalilengwa na mashambulizi hayo ya watu walioshambulia kwa risase na bomu za kurusha wakiwa kwenye pikipiki wakati waumini wa kikristo walipo kuwa makanisani.

Shambulio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Kwadakau kabla ya kuripotiwa pia katika vijiji vya Kwada, Ngurojina, Karagau na Kautikari, ambapo kundi la wanakijiji waliojitolea kwa ajili ya kujilinda walishindwa kabisa kudhibiti shambulio hilo

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...