Mazungumzo
ambayo yalitarajiwa kuanza jana baina ya waasi wa Sudani Kusini na
serikali ya rais Salva Kiir kwa lengo la kumaliza machafuko yalioanza
tangu mwezi Desemba mwaka jana, yameahirishwa hadi tarehe ambayo
hakufahamishwa na duru za upatanishi.
Hakuna
sababu zozote zilizotolewa za kuahirishwa kwa mazungumzo hayo
yaliositishwa kwa mara ya tatu tangu Mei 9, baada ya pande mbili
katika mazungumzo hayo kushindwa kuafikiana, ambapo awamu ya kwanza
ilimalizika kwa kufikia makubaliano ya kusitisha vita ambayo
hayajawahi kushimiwa.
Hata hivyo
kongamano linalo wajumuiya wajumbe wa serikali, wajumbe waasi na wale
wa mashirika ya kiraia, pamoja na taasisi za kidini linatarajiwa
kuanza hii leo alhamisi jijijni Addsi Ababa nchini Ethiopia, baada ya
kongoamano hilo huenda tarehe ya kuanza kwa mazungumzo hayo
ikatangazwa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire