Mapigano
mapya yamezuka mashariki mwa syria kati ya waasi wanaotaka rais
Bashar al-Assad aondoke madarakani na wapiganaji wa kundi la kijihadi
lililoteka baadhi ya maeneo ya mpaka kwenye nchi jirani Iraq.
Hatua
hiyo inakuja wakati umoja wa mataifa ukisema kuwa hali si shwari
nchini Syria na kwamba mgogoro huo ni tishio kwa usalama wa kanda
nzima ya mashariki ya kati.
Mwenyekiti
wa tume ya uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu wa umoja wa
mataifa Paulo Pinheiro amelieleza baraza la haki za binadamu la umoja
huo hii leo kuwa uchunguzi walioufanya nchini syria unaonyesha kuwa
kuna makaosa mengi ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Kwa
upande wake mkuu wa tume ya misaada ya kibinadamu ya umoja wa
mataifa VALERIE AMOS amesema kuwa wanakabiliwa na hali ngumu ya
kufikia maeneo yanayohitaji misaada tangu rais Bashar al-Assad
achaguliwe tena kushika wadhifa huo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire