Majadiliano
baina ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ujumbe
maalum kutoka serikali ya Congo- Brazzaville yanaingia hii leo katika
siku yake ya pili mjini Kinshasa, ikiwa ni jaribio la kupunguza
mvutano uliojitokeza kati ya nchi hizo mbili baada ya wakongo wa DRC
kufukuzwa kutoka nchi ya Congo Brazaville hivi karibuni.
Katika
kipindi cha miezi miwili iliyopita, takriban watu laki moja na elfu
arobaini wamelazimika kuvuka mpaka baada ya kufukuzwa katika
mazingira tatanishi na kuzua mgogoro wa kidiplomasia baina ya nchi
hizo jirani.
Waziri wa mambo ya ndani wa DRC na kiongozi wa ujumbe wa nchi hiyo katika majadilianao hayo Richard Muyej amekosoa na kushutumu operesheni hiyo aliyoiita kuwa ya kikatili pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa
upande wa Congo-Brazaville, msimamo ulionekana kutoyumbishwa na
shutma hizo huku wakiahidi kuendelea na operesheni hiyo huku wakizingatia taratibu za kisheria.
Raymond Zephyrin Mboulou |
Naye
Gavana wa Jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku aliyehitimisha ziara
yake katika makambi walioko raia hao wa DRC waliorejeshwa mjini
Kinshasa amesema kuwa operesheni hiyo ilikiuka haki za bianadamu na
haikubaliki.
Julien Paluku Kahongya |
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire