watu 21
wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 112 wamejeruhiwa katika
mapigano yalioibuka hapo jana kwenye mji wa Benghazi mashariki mwa
Libya, mapigano yanayodaiwa kuwa ni kati ya wapiganaji wa kundi la
Ansar al-Shariah na wapiganaji wafuasi wa kiongozi wa zamani wa
jeshi, Khalifa Haftar.
Wakazi wa
mji wa Benghazi wamethibitisha kusikia milio ya risasi kwenye mji
huo, ambapo mbali na mapigano ya Jumatatu ya wiki hii, siku ya
Jumapili pia kulishuhudiwa makabiliano kati ya makundi haya hasimu.
Mapigano
hayo yalianza pale kundi la Ansar Al Charia liliposhambulia kambi ya
kijeshimjini Benghazi lenye wapiganaji wengi waliojiunga hivi
karibuni na jenerali aliye asi Khalifa Haftar. Shmbulio hilo ni jibu
la wazi kwa jenerali huyo anaye endesha kampeni dhidi ya Uslam tangu
Mei 16.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire