Serikali ya
Marekani inaituhumu serikali ya Rwanda kuwakamata watu pasipo sababu
na kuiomba serikali ya Kigali kuheshimu uhuru wa kujieleza, jambo
ambalo limeilazimu serikali ya Rais Paul Kagame kujibu bila ya
subira.
Katika
taarifa iliyosomwa na Marie Harf, msemaji wa wizara ya mambo ya nje
wa Marekani, serikali ya rais Obama imeeleza wasiwasi wake kuhusu
kutoweka kwa idadi kubwa ya watu katika mazingira tatanishi pamoja na
vitisho vinavyoendelea dhidi ya waandishi wa habari.
Aidha,
serikali ya Marekani inaiomba Rwanda kutoa maelezo kuhusu hatma ya
raia wa rwanda waliokamatwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita
na kuitaka iheshimu haki za binadamu kwa mujibu wa sheria za Rwanda
na za kimataifa.
Onyo hilo
limekuja saa chache baada ya kiongozi wa chama upinzani nchini Rwanda
cha PS-Imberakuri Bernard Ntaganda kuachiwa huru ambapo ametumikia
kifungo cha miaka minne jela kwa tuhuma za kujenga chuki, utengano
na mifarakano nchini humo.
Akijibu
tuhuma hizo za Marekani dhidi ya serikali, Louise Mukishiwabo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda amewataka watu kuacha kutumia kila
neno au tendo litakalowatia nguvu waasi wa kihutu wa FDLR pamoja na
washirika wao na hivyo kuhatarisha maisha ya Wanyarwanda, na kwamba
nchi yake haitasita kuchukua hatuwa madhubuti za kushughulikia tishio
lolote kwa usalama wa Rwanda.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire