Rais wa kenya Uhuru Kenya amelaani mmatukio ya ulipuaji wa mabomu yaliyosababisha vifo vya wananchi wake huku kundi la Al Shabab likidai kuwa limehusika na mashambulizi hayo.
Rais
Kenyatta kwa upande wake amekanusha kuwa mashambulizi hayo yalifanywa
na kundi la kigaidi la Al shabab na kutuhumu mtandao wa kisiasa
nchini kenya kuwa unahusika na mauaji hayo.
Kenyatta Ameeleza kuwa uchunguzi wa kiintelijinsia unaonyesha kuwa shambulizi
la Lamu mjini Mombasa lilipangwa na kutekelezwa na mtandao huo wa
kisiasa unaochochea machafuko ya kikabila kwa jamii ya watu wa kenya.
Rais
Kenyatta amesema kuwa shambulizi si la al shabab bali ni mtandao wa
ndani ambao pia ulitoa nafasi kwa wahalifu kutekeleza matukio hayo
ya uhalifu dhidi ya binadamu ingawaje hakutaja moja kwa moja ni
mtandao upi unaohusika.
Kwa
upande wake mtandao wa wanaharakati wa Pwani ya Kenya umesema
wataandaa maandamano makubwa kama serikali ya kenya haitachukua hatua
kukabiliana na mashambulizi ya aina hiyo
Kwa
upande wa wachambuzi wa siasa na usalama wanaona kuwa hatua zaidi
lazima zichukuliwe kwa kuhakikisha kuwa vikosi vya usalama vinapata
vifaa vya kisasa ili kukabiliana na mashambulizi kama hayo
Shambulizi
la usiku jumapili lilisababisha vifo vya watu 50, na shambulizi la
jumatatu usiku lilisababisha vifo vya watu 15 na yote kulndi la Al
Shabab limejigamba kutekeleza huku kukiwa na taarifa za kutekwa kwa
wanawake 12.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire