Kiongozi
wa upoinzani Kenya Raila Odinga amesema chama chake hakijahusika kwa
njia yoyote ile katika mauaji ya watu zaidi ya sitini yaliotokea
nchini humo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Odinga amelaani vikali mashambulizi
yaliotekelezwa usiku wa Jumapili na lile la usiku wa Jumatatu, na
kufahamsisha kwamba muungano wa CORD unapinga katu katu mauaji kama
njia ya kufikia kwenye malengo ya kisiasa.
Licha
ya kundi la Al Shabab kukiri kuhusika na shambulio hilo, rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta alikanusha kuhusika kwa kundi hilo na kusisitia
kuwa yalitekelezwa na mtandao wa ndani wa kisiasa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire